Mjumbe maalumu wa Rais wa China ahudhuria shughuli za maombolezo ya kifo cha Emir wa Kuwait Sheikh Nawaf
2023-12-19 09:22:00| CRI

Mjumbe maalumu wa Rais wa China Bw. Shohrat Zakir jana tarehe 18 alihudhuria shughuli za maombolezo ya kifo cha Emir wa Kuwait Sheikh Nawaf Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah, na kukutana na Emir mpya wa Kuwait Sheikh Mishal Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah.

Bw. Shohrat Zakir amesema Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Emir Sheikh Nawaf kwa niaba ya serikali ya China na wananchi wake. Amesema Emir Sheikh Nawaf ametoa mchango mkubwa katika kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya China na Kuwait, na China inatilia maanani uhusiano huo na kupenda kuendelea kushirikiana na Kuwait katika kuhimiza uhusiano huo upate maendeleo mapya.

Emir Sheikh Mishal ameeleza shukrani kwa rais Xi na mjumbe wake Shohrat Zakir kutoa rambirambi hizo akisisitiza kuwa Kuwait inapenda kushirikiana na China katika kuimarisha ushirikiano kati yao katika sekta mbalimbali.