Wataalamu watoa wito wa matumizi ya teknolojia ya Juncao kuhimiza kilimo endelevu barani Afrika
2023-12-19 08:44:09| CRI

Wataalamu wanaohudhuria warsha kuhusu teknolojia ya Juncao mjini Addis Ababa, wametoa wito kwa juhudi za pamoja za matumizi ya teknolojia hiyo kuendeleza kilimo endelevu barani Afrika.

Warsha hiyo ya siku mbili imeandaliwa kwa pamoja na Ujumbe wa China kwenye Umoja wa Afrika (AU), Idara ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (UN-DESA), Kituo cha Kitaifa cha Utafiti na Uhandisi wa Teknolojia ya Juncao chini ya Chuo Kikuu cha Kilimo na Misitu cha Fujian (FAFU).

Kamishna wa AU anayeshughulikia kilimo, maendeleo ya vijijini, uchumi wa bluu na mazingira endelevu Bw. Joseph Sacko, ameeleza uungaji mkono mkubwa na utayari wa AU wa kushirikiana na China katika matumizi ya teknolojia ya Juncao kote barani Afrika.

Amesema teknolojia ya Juncao ni teknolojia ya gharama nafuu ambayo itasaidia kutambua uhakika wa chakula na kupunguza umaskini miongoni mwa watu maskini vijijini. Teknolojia hiyo imethibitishwa kwenye uzalishaji wa uyoga na malisho ya mifugo, na inatarajiwa kuchangia katika kupambana na utapiamlo barani Afrika.