Kenya yaadhimisha siku ya haki za wachache ya Umoja wa Mataifa na kuhimiza kuwepo kwa usawa
2023-12-19 08:43:20| CRI

Kenya iliungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Haki za Wachache huku kukiwa na wito wa kuhimiza usawa miongoni mwa jamii za walio wachache na waliotengwa wanaoishi nchini humo.

Maadhimisho hayo yanafanyika baada ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kupitisha tamko la haki za watu wa jamii ya watu wachache wa kitaifa au kikabila, kidini na kilugha, yamekutanisha mashirika ya Umoja wa Mataifa, wanadiplomasia na maofisa wakuu wa serikali, kujadili njia za kuondoa ubaguzi dhidi ya makundi ya walio wachache.

Katibu mkuu wa baraza la mawaziri ambaye pia ni katibu wa baraza la mawaziri wa maswala ya kigeni na diaspora Bw. Musalia Mudavadi, aliwaambia wanahabari mjini Nairobi kuwa Kenya inaendelea kuwa na nia ya kuwasaidia watu wa makabila madogo kupitia uingiliaji unaolenga kuwawezesha kiuchumi.