Mahakama ya Katiba nchini Uganda yaanza kusikiliza kesi zinazopinga sheria ya wapenzi wa jinsia moja
2023-12-19 13:49:31| cri

Mahakama ya Katiba nchini Uganda jana imeanza kusikiliza kesi zinazopinga sheria tata ya wapenzi wa jinsia moja inayotoa adhabu ya kifo na kifungo cha maisha jela kwa vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

Jopo la majaji watano likiongozwa na Naibu Jaji Mkuu Richard Buteera limepokea malalamiko na pingamizi kutoka kwa wanaharakati wanaotetea mapenzi ya jinsia moja na mashirika ya kiraia yanayotaka sheria hiyo mpya iliyosainiwa na rais wa Uganda, Yoweri Museveni mwezi Mei mwaka huu, kuwa ni batili.

Kutokana na maelekezo ya mahakama hiyo, pande zote ziliwasilisha nyaraka za maandishi na kukubali kutotambulisha nyaraka nyingine mpya ama mashtaka mapya wakati kesi hiyo ikisikilizwa.