Idadi ya vifo katika tetemeko la ardhi huko Gansu nchini China yaongezeka hadi 111
2023-12-19 09:06:26| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa maagizo kuhusu kuanzisha uokoaji kwa pande zote na kuwapanga watu waliokumbwa na tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 6.2 kwenye kipimo cha Richter lililotokea jana jioni wilayani Jishishan mkoa wa Gansu na kusababisha vifo vya watu 111.

Habari zinasema tetemeko hilo pia limesababisha vifo vya watu tisa na kuwajeruhi wengine 124 katika mji jirani wa Haidong mkoani Qinghai.

Makao makuu ya kushughulikia dharura ya tetemeko la ardhi ya Baraza la Serikali ya China, pamoja na Wizara ya Usimamizi wa Mambo ya Dharura zimetuma kikosi kazi kwenye maeneo yaliyokumbwa na tetemeko hilo.

Wizara hiyo imewasiliana na idara ya tetemeko la ardhi ya China na mamlaka za mitaa ili kupata habari mpya kuhusu tetemeko hilo, pia inaongoza kazi za utafutaji na uokoaji kwenye maeneo yaliyoathirika.