Umoja wa Afrika watoa mwito kusimamisha vita mara moja nchini Sudan
2023-12-19 09:29:38| CRI

Umoja wa Afrika umeeleza wasiwasi kuhusu hali ya usalama inayozidi kuwa mbaya nchini Sudan, huku ukitoa mwito pande husika katika nchi hiyo kusimamisha vitendo vya uhasama.

Mwenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat ametoa taarifa akieleza wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa mapigano nchini humo.

Taarifa hiyo imesema mwenyekiti huyo amesikitishwa na uwepo wa majerahi wengi wa Darfur, ambao katika miaka 20 iliyopita waliishi huko Abu Shok kwenye eneo la kuwahifadhi, lakini mapigano yametokea tena katika siku kadhaa zilizopita.

Kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama nchini Sudan, Bw. Faki ameeleza ufuatiliaji juu ya ripoti za hivi karibuni kuhusu mashambulizi yaliyofanywa tena dhidi kambi ya Abu Shouk inayohifadhi wakimbizi wa ndani, pamoja na mapigano yaliyoenea katika eneo la Wad Medani jimboni Gezira.