Waziri mkuu wa Rwanda akutana na Mu Hong
2023-12-19 09:28:34| CRI

Waziri mkuu wa Rwanda Bw. Édouard Ngirente amekutana mjini Kigali na naibu mwenyekiti wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la China ambaye pia ni mkuu wa kikundi cha urafiki kati ya China na Afrika cha baraza hilo Bw. Mu Hong.

Bw. Mu amefikisha salamu za rais Xi Jinping wa China kwa mwenzake wa Rwanda Paul Kagame, na salamu za waziri mkuu wa China Bw. Li Qiang kwa Bw. Ngirente, na kusema uhusiano kati ya nchi mbili una historia ndefu, China siku zote inachukulia na kuendeleza uhusiano kati ya nchi mbili na kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi mbili kwa manufaa ya watu wa nchi hizo. Bw. Mu pia amejulisha hali kuhusu usasa wenye mtindo wa kichina na ujenzi wa pamoja wa“Ukanda Mmoja na Njia Moja”.

Bw. Ngirente ameshukuru uungaji mkono wa China kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Rwanda, na kusema China ni mwenzi wa kuaminika kwa Rwanda na nchi nyingine za Afrika, na Rwanda itaendelea kuhimiza kwa ufanisi na kasi ushirikiano kati ya pande mbili.