Tanzania kushirikiana na China masuala ya uhamiaji
2023-12-19 13:48:57| cri

China imesaini mkataba wa makubaliano na Tanzania kwa ajili ya kuimarishwa uhusiano kati ya Jeshi la Uhamiaji la Tanzania na la China.

Makubaliano hayo yamefanyika katika Chuo cha Uhamiaji Moshi na kuhudhuriwa na maofisa wa Jeshi la uhamiaji kutoa China na Tanzania. Akizungumza jana Jumatatu Desemba 18, 2023 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Jumanne Sagini, alisema makubaliano hayo ni matokeo ya ziara ya Rais Samia Suluhu Hassani aliyoifanya nchini China.

Amesema makubaliano hayo, yatasaidia Tanzania kujifunza nchini China, kutokana na nchi hiyo kufanya vizuri katika idara ya uhamiaji, pia itasaidia kukuza viwanda kutokana na nchi hiyo kufanya vizuri katika sekta ya viwanda duniani.

Naye kamishna wa uhamiaji nchini China, Li Junjie amesema makubaliano yaliyoingiwa ni kutokana na uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na China.