China yafanya mkutano mkuu wa kazi za vijijini
2023-12-20 20:29:54| cri

Mkutano mkuu wa kila mwaka wa kazi za vijijini ulifanyika Beijing siku ya Jumanne na Jumatano, ukiainisha vipaumbele vya kazi za vijijini mnamo 2024.

Xi Jinping, katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, rais wa China na mwenyekiti wa Tume Kuu ya Kijeshi, alitoa maagizo muhimu kuhusu kazi zinazohusiana na kilimo, maeneo ya vijijini na wakulima.