Ubalozi wa China waikabidhi Somalia dola za kimarekani zaidi ya milioni moja kusaidia wahanga wa mafuriko
2023-12-20 08:52:21| CRI

Ubalozi wa China nchini Somalia umeikabidhi serikali ya Somalia msaada wa kibinadamu wa dola za kimarekani zaidi ya milioni moja kusaidia wahanga wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni nchini humo.

Balozi wa China nchini Somalia Fei Shangchao amesema msaada huo unatarajiwa kuleta ahueni kwa wahanga hao. Kamishna wa shirika la usimamizi wa maafa la Somalia Bw. Mohamud Moallim Abdulle ameshukuru msaada huo kutoka China.

Kutokana na takwimu zilizotolewa na serikali ya Somalia, mafuriko katika maeneo ya kusini na kati mwa nchi hiyo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya mia moja na wengine milioni 1.7 kukimbia makazi yao.