Mamlaka ya bandari Tanzania yafungua ofisi Malawi ili kurahisisha biashara
2023-12-20 08:23:26| CRI

Mamlaka ya bandari Tanzania (TPA) imefungua ofisi mjini Lilongwe nchini Malawi ili kurahisisha biashara kati ya nchi hizo mbili kupitia bandari ya Dar es Salaam.

Maneja mkuu wa TPA Bw. Plasdure Mbossa amesema ofisi hiyo itafanya kazi kuunganisha wadau wote wa Bandari ya Dar es Salaam katika usafirishaji wa mizigo kwa wateja nchini Malawi, akiongeza kuwa ofisi hiyo pia itawajibika na kutoa mapendekezo kuhusu mawakala wanaoaminika wa ushughulikiaji wa mizigo bandarini.

Kwa mujibu wa ofisa huyo majukumu mengine ya ofisi hiyo ni pamoja na utoaji wa habari zinazohitajika kuhusu mizigo inayoagizwa kwenda Malawi kupitia bandari za Dar es Salaam, Mbamba Bay, na Kyela nchini Tanzania.