Celine Dion apoteza uwezo wa kudhibiti misuli yake kufuatia kukabiliwa na ugonjwa wa kukakamaa “Stiff-Person Syndrome”
2023-12-20 22:57:15| cri

Mwimbaji wa Canada Celine Dion amewatia mashabiki wake wasiwasi kutokana na taarifa mpya za afya yake zilizotangazwa na dada yake Claudette Dion.

Hivi karibuni Claudette alisema dada yake amepoteza udhibiti wa misuli yake na kinachomuumiza moyo ni kwamba siku zote amekuwa na nidhamu na amekuwa akifanya kazi kwa bidii. Mama yao alimwambia kila mara kwamba atafanya vizuri na kwa usahihi.

Ameendelea kusema kwamba ndoto zao na za Celine ni kurejea tena jukwaani. Dada mwingine wa Celine, Linda, anaishi naye huko Las Vegas, Marekani, anapopatiwa matibabu na madaktari waliobobea katika ugonjwa wa kukakamaa “Stiff-Person Syndrome”.

Muda mfupi baada ya kusambaa kwa taarifa za afya ya nyota huyo, mashabiki wake wengi duniani walimtakia apone haraka, na pia walisema wataendelea kumuombea dua.