Waliokufa kwa mafuriko wafikia 174 Kenya
2023-12-20 09:04:19| CRI

Msemaji wa serikali ya Kenya Bw. Isaac Mwaura amesema idadi ya vifo kutokana na mvua kubwa na mafuriko nchini Kenya imeongezeka hadi 174.

Msemaji huyu amewaambia wanahabari mjini Nairobi kuwa licha ya mafuriko kutulia, watu sita wamefariki katika siku tatu zilizopita kutokana na maporomoko ya ardhi yanayohusiana na mafuriko.

Bw. Mwaura amesema kituo cha taifa cha kukabiliana na dharura za El Nino kinaendelea kufuatilia kwa karibu hali ya mafuriko kwa kushirikiana na mashirika husika na mamlaka za mitaa, ili kupunguza athari za matukio haya ya hivi karibuni.