Ufanisi wa uchumi wa Tanzania kwa mwaka 2023 ulikuwa ni wa kuridhisha
2023-12-20 08:34:35| CRI

Benki kuu ya Tanzania imesema ufanisi wa uchumi wa Tanzania kwa mwaka 2023 ulikuwa wa kuridhisha licha ya athari za mshtuko wa dunia.

Benki hiyo imesema katika taarifa yake iliyotolewa Jumanne kuwa mwaka kesho ufanisi wa uchumi unatarajiwa kuimarika kutokana na utekelezaji wa sera za kuchochea ukuaji na kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi.

Ukuaji katika robo ya kwanza na ya pili ya mwaka 2023 ulikuwa asilimia 5.4 na asilimia 5.2 mtawalia, ukiimarishwa kwa uwepo wa aina mbalimbali za shughuli za kiuchumi. Ukuaji katika shughuli za kiuchumi pia ilionekana Zanzibar, kutokana na kuimarika kwa utalii na uwekezaji wa umma na binafsi.

Habari pia zinasema benki ya dunia imeipongeza Tanzania kwa kuwa na ongezeko imara la kiuchumi na kuzipita nchi nyingi zinazoendelea, lakini benki hiyo imesema Tanzania inatakiwa kujikita zaidi kwenye sekta binafsi ili kuwa na ukuaji zaidi katika miaka ijayo.