Zambia yakamata raia wa Uingereza akiwa na kilo 5.7 za cocaine
2023-12-20 08:24:04| CRI

Idara ya kupambana na dawa za kulevya ya Zambia imemkamata raia mmoja wa Uingereza mwenye asili ya Tanzania (64) akiwa na kilo 5.7 za cocaine.

Mshukiwa huyu alikamatwa jana Jumanne kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Simon Mwansa Kapwepwe mjini Ndola, akijaribu kuingia kwenye ndege ya kwenda Ujerumani.

Ofisa mahusiano wa Kamisheni ya Kupambana na Dawa za Kulevya (DEC) nchini Zambia, Bw. Mwenge Mulenga amesema mshukiwa huyo ambaye alituhumiwa kwa uhalifu nchini Uingereza, alishukiwa kuhusiana na kundi moja la kimataifa la dawa za kulevya linalofanya shughuli nchini Tanzania na Ujerumani.