Tshisekedi atishia kuivamia Rwanda
2023-12-20 13:58:04| cri

Katika fainali kali ya kampeni kabla ya uchaguzi wa leo Jumatano, Rais Felix Tshisekedi wa DRC alitishia kuvunja uhusiano wake wa kidiplomasia na Rwanda na kutangaza vita iwapo atachaguliwa tena. Akihutubia umati wa wafuasi wake mjini Kinshasa, sauti ya Tshisekedi ilijaa huzuni kutokana na madai ya miaka mingi ya Wanyarwanda kuingilia mashariki mwa Kongo.

"Tumevamiwa vya kutosha na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Kigali!" Tshisekedi alinguruma, huku akishangiliwa kwa maneno kama "Kagame aende! (Kagame out!)"

"Mkinichagua tena, na Rwanda ikiendelea na uchokozi wake, nitaomba Bunge na Baraza la wawakilishi waidhinishe kutangaza vita. Tutaandamana kuelekea Kigali. Mwambie Kagame, zile siku za kucheza na viongozi wa Kongo zimepita. Sitavumilia uchokozi wake!" alisema Tshisekedi.

Hata hivyo Kigali inakanusha vikali kuhusika katika mizozo ya mashariki mwa Kongo.