Uchumi wa Kenya wakadiriwa kukua kwa asilimia 5.5 mwaka 2024
2023-12-21 09:07:19| CRI

Wizara ya fedha ya Kenya imesema kuwa uchumi wa Kenya utakua kwa asilimia 5.5 mwaka w2024.

Wizara hiyo imesema katika taarifa yake ya sera ya bajeti kwa mwaka 2024 kwamba ukuaji wa uchumi utaungwa mkono na ukuaji endelevu wa sekta za huduma, kufufuka kwa sekta ya kilimo, na utekelezaji wa hatua za kukuza shughuli za kiuchumi katika sekta za kipaumbele zilizotajwa na serikali.

Taarifa hiyo imesema uchumi unatarajiwa kuendelea kukua kwa nguvu na kuongezeka kwa asilimia 5.5 mwaka 2023 na 2024, na asilimia 5.4 mwaka 2025.