Rais wa Jamhuri ya Kongo azindua jumba la maduka lililojengwa na China
2023-12-21 08:14:00| CRI

Rais wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso jana Jumatano mjini Brazzaville alizindua jumba jipya la maduka linaloaminika kuwa ni kubwa zaidi nchini humo.

Jumba hilo la maduka liitwalo “Brazza Mall”, liko kwenye eneo la Mpila na limejengwa na kampuni ya ujenzi ya China Jiangsu International kwenye eneo lililokuwa kambi ya jeshi iliyoharibiwa na milipuko mwezi Machi mwaka 2012.

Akiongea kwenye uzinduzi wa jumba hilo, meya wa Brazzaville, Dieudonne Bantsimba amesema jumba hilo litakuwa kituo cha kiuchumi na kitalii ambako shughuli za kibiashara zitaendelezwa.