Wenza wenye bahati wanusurika kwenye ajali za ndege mbili tofauti ndani ya siku moja: "Tuna Bahati"
2023-12-21 14:32:27| cri

Wenza wawili wanajihesabu kwamba wana bahati baada ya kunusurika katika ajali tofauti za ndege ndani ya siku moja. Stefano Pirilli, 30, hakujeruhiwa baada ya masaibu hayo, huku mwenza wake Antonietta Demasi mwenye umri wa miaka 22, ambaye ni mwanafunzi, aliumia kidogo wakati ndege yake ilipoanguka.

Ripoti ya Daily Mail ilifichua kwamba wenza hao waliamua kupanda ndege tofauti na kwenda kukutana na marafiki zao kwa ajili ya chakula cha mchana, wakati mkasa huo wa nadra sana ulipowakumba.

Ndege ya Pirilli yenye viti viwili ya Tecnam P92 Echo Super ilianguka San Gillio baada ya kukumbwa na matatizo, huku ndege ya Demasi ikianguka umbali wa kilomita 40 huko Busano. Madaktari wanaomhudumia Demasi walisema alikuwa na majeraha ya nyonga huku rubani wa ndege yake akitibiwa jeraha la kichwa. Prilli, mshauri wa Nishati, hakujeruhiwa, huku rafiki yake na rubani wakiripotiwa kupata majeraha kidogo.