Radi yawaua watu wanne magharibi mwa Tanzania
2023-12-21 09:00:46| CRI

Polisi wa Tanzania wamethibitisha kuwa watu wasiopungua wanne wamekufa na wengine wanane wamejeruhiwa baada ya kupigwa radi Jumanne wiki hii huko wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, magharibi mwa nchi hiyo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma Philemon Makungu amewaambia wanahabari kwamba wahanga hao walikutwa na msiba huo saa moja na nusu jioni ya Jumanne katika kijiji cha Buyezi wakiwa wamejikinga mvua katika mgahawa mmoja.