Jeshi la Somalia lakamata tena mji muhimu ulioko katikati ya Somalia kutoka kwa wapiganaji wa kundi la al-Shabaab
2023-12-21 08:54:06| CRI

Jeshi la Somalia likiungwa mkono na vikosi vya huko limekamata tena mji wa Masagaway ulioko kwenye eneo la Galguduud, jimbo la kati la Galmudug kutoka kwa wapiganaji wa kundi la al-Shabaab baada ya operesheni.

Naibu waziri wa habari, utamaduni na utalii wa Somalia Bw. Abdirahman Yusuf Al-Adala amesema vikosi hivyo vimefanikiwa kukomboa mji huo wa kimkakati kutoka kwa kundi la al-Shabaab, kufuatia mfululizo wa mashambulizi ya kijeshi.

Bw. Al-Adala amesema magaidi wa kundi la al-Shabaab wamefukuzwa kutoka mji wa Masagaway na hivi sasa operesheni za kuwasaka zinaendelea katika sehemu ya mashariki ya Galguduud.