Uganda yaimarisha usalama kabla ya msimu wa sikukuu baada ya shambulio linaloshukiwa kutekelezwa na kundi la waasi
2023-12-21 14:23:43| cri

Uganda imeimarisha usalama kabla ya msimu wa sikukuu baada ya shambulio linaloshukiwa kufanywa na waasi kusababisha vifo vya watu 10 katika wilaya ya Kamwenge, magharibi mwa nchi hiyo jumanne wiki hii.

Kwa mujibu wa Polisi nchini humo, raia 10 waliuawa katika wilaya hiyo na watu wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa kundi la ADF lenye maskani yake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Msemaji wa Jeshi la Polisi la Uganda, Fred Enanga amesema katika taarifa yake kuwa, vikosi vya pamoja vya usalama vimepelekwa kufanya doria katika maeneo yaliyoainishwa ili kuhakikisha amani, usalama, na utulivu kabla ya sikukuu ya Krismas.