Mageuzi ya reli ya Kenya yachochea maendeleo ya kisasa ya nchi hiyo
2023-12-21 10:37:38| CRI


U hali gani msikilizaji na karibu tena kwenye kipindi cha Daraja kinachokujia kila jumapili muda kama huu kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.

Miongoni mwa mambo tuliyokuandalia katika kipindi cha leo ni pamoja na habari mbalimbali kuhusu China na nchi za Afrika, pia tutakuwa na ripoti inayohusu mageuzi ya reli ya Kenya yanavyochochea maendeleo ya kisasa ya nchi hiyo, lakini pia tutakuwa na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi yatayozungumzia kukamilika kwa "Mradi wa Twinkle Star".