UNFPA: Ethiopia yaendelea kukabiliana na mahitaji makubwa ya kibinadamu
2023-12-22 09:01:34| CRI

Shirika la Idadi ya watu la Umoja wa Mataifa UNFPA, limesema Ethiopia inaendelea kukabiliana na mahitaji makubwa ya kibinadamu yanayotokana kwa kiasi kikubwa na athari mbalimbali, ikiwemo vurugu za kikabila, milipuko ya magonjwa, mapigano na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Shirika hilo limetoa ripoti kuhusu hali mpya ikisema, katika wiki kadhaa zilizopita, matukio mabaya kama vile ukame na mafuriko yameendelea kusababisha uharibifu mkubwa ikiwa ni pamoja na watu kulazimika kukimbia makazi, uharibifu wa mazao ya kilimo na njia za kujipatia riziki, huku yakisababisha ongezeko la hatari za afya na ulinzi.

Kwa mujibu wa shirika hilo watu milioni 5 wanaripotiwa kuathiriwa na hali ya ukame katika majimbo ya Amhara na Tigray.