Balaa katika mbuga ya Zimbabwe: Tembo wanahaha kutafuta maji
2023-12-22 13:31:42| cri

Mawingu ya dhoruba hatimaye yanatanda kwenye hifadhi kubwa zaidi ya wanyama nchini Zimbabwe, lakini yamechelewa sana kwani zaidi ya tembo 110 wamekufa kutokana na ukame mkali.

Walinzi wa Hifadhi ya Taifa ya Hwange hawana la kufanya isipokuwa kukata pembe za mizoga ya tembo kabla majangili kuzipata.

Wakati mawingu meusi katika siku za hivi karibuni yakionesha dalili za mvua za kuokoa maisha, walinzi hao wanaweza wasipate tembo wote waliokufa kutokana na ukame kwenye uwindaji wao wa kila siku.

Mbuga hiyo yenye urefu wa kilomita za mraba 14,600 (maili 5,600 za mraba) ni kubwa kuliko za nchi nyingi na ina tembo zaidi ya 45,000 wa savanna, wengi sana hadi wanachukuliwa kuwa tishio kwa mazingira.