Mkuu wa jeshi la Sudan akataa makubaliano ya amani bila kuondoka kwa vikosi vya wanamgambo
2023-12-22 08:24:12| CRI

Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan jana Alhamisi alisema jeshi lake halitasaini makubaliano yoyote ya amani yasiyohusisha kuondoka kwa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kutoka kwenye miundombinu ya umma na nyumba za raia.

Bw. Al-Burhan ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Mpito la Sudan, alitoa kauli hiyo alipohutubia maofisa na askari katika jimbo la mashariki la Red Sea.

Bw. Al-Burhan amesema makubaliano yoyote yanatakiwa kuhusisha usitishwaji vita na kuondoka kwa waasi kutoka kwenye miundombinu ya umma, hospitali na nyumba za raia, akiongeza kuwa Jeshi la Sudan litaendelea na mapambano mpaka kuwashinda “wanamgambo waasi”.