Chad yapitisha marekebisho ya katiba kwa asilimia 86 ya kura
2023-12-25 22:58:50| cri

Tume ya Uchaguzi nchini Chad imetangaza kuwa, matokeo ya awali ya kura za marekebisho ya katiba nchini humo yameonyesha kuwa, wapiga kura wamepitisha marekebisho ya katiba hiyo kwa asilimia 86.

Viongozi wa kijeshi nchini humo walipendekeza marekebisho ya katiba kama hatua muhimu katika njia ya kurejesha utawala wa kiraia, hatua ambayo imepingwa na wanasiasa wa upande wa upinzani.