Israel yashambulia kambi ya wakimbizi iliyoko katikati ya Gaza na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 70
2023-12-25 09:08:01| CRI

Habari kutoka kituo cha televisheni cha Palestina imesema wapalestina wasiopungua 70 wameuawa kwenye shambulizi la  kutoka angani lililofanywa na Israel siku ya Jumapili kwenye kambi ya wakimbizi ya al-Maghazi iliyoko katikati ya Ukanda wa Gaza.

Msemaji wa Wizara ya Afya huko Gaza Bw. Ashraf Al-Qedra alitoa taarifa akisema, idadi ya vifo inaweza kuongezeka kwa kuwa shambulizi hilo lilipiga kwenye  lililenga sehemu yenye wakazi wengi. Aliongeza kuwa jeshi la Israel linashambulia barabara kuu za mkoa wa kati zinazopitia maeneo ya kambi, hali ambayo inazuia usafiri wa magari ya wagonjwa na magari mengine ya raia kufika maeneo yaliyolengwa.

Habari zinasema wengi waliouawa ni wanawake na watoto, na kwa sasa ni vigumu kwa hospitali za huko kuwapokea majeruhi wengi zaidi. Licha ya kambi ya wakimbizi ya al-Maghazi, jeshi la Israel lilishambulia kambi ya al-Bureij iliyoko katikati ya Gaza na mji wa kusini wa Khan Younis.