Watu 160 wauawa katika mashambulio katikati ya Nigeria
2023-12-26 23:13:22| cri

Makundi yenye silaha yamewaua watu 160 katikati ya Nigeria katika mfululizo wa mashambulio dhidi ya vijiji.

Maofisa wa serikali ya eneo hilo wamesema jana kuwa, idadi hiyo imeongezeka kutoka ile iliyoripotiwa na jeshi la nchi hiyo jumapili jioni, kwamba ni watu 16 tu ndio wameuawa katika eneo hilo linalokabiliwa na mvutano wa kidini na kikabila uliodumu kwa miaka kadhaa.