Waziri mkuu wa China atoa wito wa maendeleo jumuishi na ushirikiano wa usalama miongoni mwa nchi za eneo la Lancang-Mekong
2023-12-26 09:07:32| CRI

Waziri mkuu wa China Li Qiang ametoa wito kwa nchi za eneo la Lancang-Mekong kuimarisha maendeleo jumuishi na ushirikiano wa usalama, akitangaza uamuzi wa China wa kutoa mkopo maalumu kwa ajili ya maendeleo ya pamoja kwa nchi hizo.

Li alisema hayo Jumatatu kwenye mkutano wa nne wa viongozi wa Ushirikiano wa nchi za eneo la Lancang-Mekong (LMC) ulioongozwa naye na kiongozi wa Myanmar Min Aung Hlaing kwa njia ya video, akitaka nchi hizo sita kuweka mfano wa kuigwa katika ujenzi wenye kiwango cha juu wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Dunia, Mpango wa Usalama wa Dunia, na Mpango wa Ustaarabu wa Dunia iliyotolewa na rais Xi Jinping wa China.

Li pia amependekeza nchi hizo kutekeleza miradi ya pamoja ya kuhimiza mawasiliano na ushirikiano wao katika sekta mbalimbali zikiwemo biashara, uzalishaji wa viwanda, kilimo, maendeleo ya kijani n.k.