Rais wa Iran aomboleza kifo cha kamanda wa IRGC aliyeuawa kwenye shambulizi la Israel nchini Syria
2023-12-26 09:01:01| CRI

Rais Ebrahim Raisi wa Iran ametoa salamu za rambirambi kwa familia ya kamanda wa Jeshi la Ulinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) Seyyed Razi Mousavi kufuatia kifo chake kwenye shambulizi la kombora lililofanywa na Israel huko Damascus, mji mkuu wa Syria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tovuti ya ofisi ya Rais, kiongozi huyo amesema kitendo chenye nia mbaya cha Israel kinaonyesha tena udhaifu wake, unyonge wake na kukata tamaa kwenye eneo hilo, na kuapa kuwa Israel itaadhibiwa kwa makosa yake.