Wizara ya Afya yenye makao yake Gaza imetangaza kuwa takriban Wapalestina 20,674 wameuawa, na wengine 54,536 kujeruhiwa katika mzozo unaoendelea kati ya Israel na Hamas tokea Oktoba 7.
Wizara hiyo Jumatatu ilisema katika muda wa saa 24 zilizopita, Wapalestina 250 walikufa katika mashambaulizi 25 kutoka anga na ardhini yaliyofanywa na vikosi vya Israel dhidi ya eneo lote.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina iliilaani Israel kwa kupuuza wito wa kimataifa wa kusitishwa kwa mashambulizi ya kijeshi dhidi ya raia wa Palestina na kuwazuia wanamgambo walowezi.
Wakati huo huo, wizara hiyo imesisitiza haja ya kupitishwa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kusitisha mapigano ili kuruhusu utolewaji wa msaada ulio salama na wa haraka na kuhakikisha usalama wa raia wa Palestina.