Ikiwa kwenye hatari ya kuzorota kwa uchumi, Uingereza imeshuhudia mwaka 2023 ukiwa mbaya sana kwa uchumi wake, na mwaka ujao hauonekani kuwa mzuri pia.
Mfumuko wa bei nchini humo umekuwa wa juu kwa zaidi ya miaka miwili, na kufanya mzozo wa gharama za maisha kuwa mada kubwa nchini kote. Kiashiria cha Bei ya Mlaji (CPI) kilipanda kwa asilimia 3.9 katika kipindi cha miezi 12 hadi Novemba 2023, hasa kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta na kupanda polepole kwa bei za vyakula.
Kiwango hiki ni cha chini zaidi tangu Septemba 2021, kutoka kiwango cha juu cha miaka 41 cha asilimia 11.1 cha mwezi Oktoba 2022. Kushuka kwa mfumuko wa bei kulikaribishwa na familia na wafanyabiashara nchini. Hata hivyo kushuka huko hakumaanishi bei ya chini, isipokuwa unapanda sio haraka sana tu.
Mchumi kutoka Mfuko wa Washauri Bingwa wa Resolution, Lalitha Try, anasema kiwango kikubwa na muda wa msukosuko wa gharama za maisha inamaanisha kwamba kauli zozote za ushindi katika vita vya kudhibiti mfumuko wa bei ni za mapema, kwani familia bado zinakabiliwa na shida.