Waathirika wa mafuriko katika Kaunti ya Lamu nchini Kenya wapokea msaada
2023-12-26 10:14:07| cri

Waathirika wa mafuriko wanaoishi katika Kaunti ya Lamu nchini Kenya wamepokea fedha na misaada mingine ya kibinadamu.

Kwa mujibu wa ripoti ya serikali ya Kaunti ya Lamu  kuhusu janga la El-Nino, jumla ya familia 2,599 zimeathiriwa na mafuriko, ambapo familia 822 hazina makazi baada ya nyumba zao kuharibiwa na mafuriko hayo.

Kaunti ya Lamu ina karibu kambi 12 za waathirika waliohama vijijini kwao baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko, zikiwemo Moa, Kitumbini, Lumshi A na B, na Mikinduni B.