UM waonya kutokea kwa mgogoro mbaya wa kibinadamu wakati Israel ikiongeza mashambulizi ya ardhini katikati ya Gaza
2023-12-27 10:01:18| CRI

Israel imetangaza kuongeza mashambulizi yake ya ardhini katika maeneo ya katikati ya Ukanda wa Gaza huku Umoja wa Mataifa ukionya kuwa kuongezeka kwa mashambulizi kutasababisha migogoro ya kibinadamu kuwa mikubwa zaidi katika Ukanda huo ambao umeharibiwa sana na vita.

Msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Bw. Seif Magango amesema kwenye taarifa kuwa mashambulizi zaidi ya 50 yamefanywa katikati ya Gaza tarehe 24 na 25 mwezi huu, yakilenga kambi za wakimbizi ya Bureij, Nuseirat na Maghazi na kati yao mashambulizi mawili yameharibu majengo saba ya makazi na kuwaua watu wasiopungua 86.