Kundi la Houthi la Yemen latangaza kuhusika na mashambulizi dhidi ya meli ya kibiashara kwenye Bahari ya Shamu katika mji wa Israel
2023-12-27 10:00:12| CRI

Kundi la waasi la Houthi nchini Yemen limetangaza kuhusikana na mashambulizi mapya dhidi ya meli moja ya kibiashara ijulikanayo kama MSC UNITED katika Bahari ya Shamu mjini Eilat, Israel, kaskazini mwa Bahari hiyo.

Msemaji wa vikosi vya Houthi Yehya Sarea ametoa taarifa hiyo kwenye televisheni ya al-Masirah inayoendeshwa na kundi hilo na kuongeza kuwa vikosi vya Houthi pia vilifanya shambulizi jingine dhidi ya mji wa Eilat wa Israel, kwa kutumia droni nyingi za kujitoa muhanga.

Kwa sasa hakuna habari yoyote kuhusu idadi ya wahanga na uharibifu kwenye mashambulizi hayo mawili.