Meli yalipuka mjini Mombasa, Kenya
2023-12-27 10:10:53| cri

Mtu mmoja amejeruhiwa katika mlipuko uliotokea ndani ya meli ya mafuta iliyokuwa imetia nanga karibu na kituo cha meli cha African Marine kilichoko Liwatoni, Likoni, mjini Mombasa, Kenya.

Akithibitisha tukio hilo, Mkuu wa Polisi wa kituo cha Central, Bw. Maxwel Agoro, amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mlipuko huo ulisababishwa na mrundikano wa gesi ndani ya matangi ya kusafirisha mafuta yaliyokuwa ndani ya meli hiyo.

Mlipuko huo mkubwa ulitetemesha majengo yaliyokuwa umbali wa kilomita mbili kutoka kwenye eneo la tukio, na kusababisha moto ulioharibu sehemu za meli hiyo.

Hata hivyo, hatua za haraka zilizochukuliwa na Mamlaka ya Bandari Kenya (KPA) kwa kupeleka maboti na magari ya zimamoto zilizuia uharibifu zaidi.