Watu wasiopungua 20 wauawa katika shambulizi la Israel dhidi ya jengo moja kusini mwa Gaza
2023-12-28 09:10:52| CRI

Wizara ya Afya ya Gaza imesema shambulizi la mabomu lililofanywa na Israel Jumatano dhidi ya jengo moja lilioko karibu na hospitali katika mji wa Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza limesababisha watu wasiopungua 20 kuuawa na wengine makumi kujeruhiwa.

Msemaji wa wizara hiyo Bw. Ashraf al-Qedra amesema kwenye taarifa kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka wakati waokoaji wakitafuta manusura chini ya vifusi vya jengo hilo.

Vyanzo vya ndani vya habari vimeliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kuwa wakati shambulizi lilipotokea walikuwepo Wapalestina wengi wasio na makazi kwenye jengo hilo.