CMG kutoa filamu ya kumbukumbu kuhusu ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika Kusini
2023-12-28 10:54:07| cri

Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) litatoa filamu ya kumbukumbu kuhusu ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika Kusini, ikiwa ni maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili.

Filamu hiyo inaanzia na ziara rasmi ya nne ya Rais Xi Jinping wa China nchini Afrika Kusini, na kueleza matokeo ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali za mambo ya kidiplomasia, uchumi na mawasiliano ya watu kwa watu.