Senegal yazindua mtandao wa kwanza wa mabasi ya umeme ya mwendo kasi Afrika kusini mwa Sahara
2023-12-28 09:07:53| CRI

Senegal imezindua mtandao wa kwanza wa mabasi ya umeme ya mwendo kasi (BRT) Afrika kusini mwa Sahara katika mji mkuu Dakar.

Mradi huo wa Dakar BRT, ambao una jumla ya urefu wa kilomita 18.3 na vituo 23 vya mabasi na vituo vitatu vya kubadilisha mabasi, ulijengwa na Kampuni ya CRBC ya China. Mabasi yote ya umeme kwenye mradi huo yametolewa na kampuni ya CRRC ya China.