Umoja wa mabalozi wa nchi za Afrika nchini Tanzania watoa msaada kwa waathirika wa mafuriko Hanang
2023-12-28 22:52:09| cri

Umoja wa Mabalozi wa nchi za Afrika wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania umekabidhi msaada wa mifuko 1,000 ya saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa nyumba za wananchi waliokumbwa na mafuruko na maporomoko ya udongo katika eneo la Katesh wilayani Hanang Mkoa wa Manyara nchini humo.

Akikabidhi msaada huo kwa Serikali, Kiongozi wa Mabalozi hao na Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Tanzania, Dk. Ahamada El Badaoui Mohamed amesema Umoja huo umesikitishwa na mafuriko yaliyotokea Katesh na kutoa msaada wa mifuko 1,000 ya saruji kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa majanga hayo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa nchini Tanzania, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk aliyepokea msaada huo kwa niaba ya Serikali, amewashukuru mabalozi hao kwa umoja wao na kwa msaada huo ambao utasaidia kurejesha makazi ya wananchi wa Katesh.