Bunge lapinga vifungu hasi kuhusiana na China kwenye muswada wa uidhinishaji wa ulinzi wa Marekani
2023-12-28 09:08:56| CRI

Msemaji wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Umma la China Xu Dong ameeleza kutoridhishwa na kupinga vikali kwa vifungu hasi vinavyohusiana na China katika Muswada wa Uidhinishaji wa Kitaifa wa Ulinzi wa Marekani kwa mwaka wa fedha wa 2024, ambao umetiwa saini kuwa sheria hivi karibuni.

Alisema sheria hiyo inachezea suala la Taiwan, kutetea ushindani wa kimkakati dhidi ya China, kuielezea China kama tishio, na kuhimiza “kuondoa hatari” kwenye sekta muhimu kwa China.

Ameongeza kuwa Marekani inaingilia vibaya mambo ya ndani ya China, kudhalilisha vikali mamlaka, usalama na maslahi ya maendeleo ya China, na kwenda kinyume na makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa China na Marekani kwenye mkutano wa San Francisco.