Mchango wa China katika dunia inayokabiliwa na changamoto mbalimbali
2023-12-29 10:13:13| cri

Mchango wa China katika ujenzi wa amani ya dunia

Nafasi ya China katika kukabiliana na mgogoro wa Israel na Palestina imetambuliwa vizuri na jamii ya kimataifa. Ikiwa nchi mwenyekiti wa zamu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu wa Novemba, China imechukua hatua za kivitendo kuondoa mvutano na kujenga maafikiano. Matokeo yake, ikiwa ni siku zaidi ya 40 tangu mapigano mapya kati ya Israel na Palestina yatokee, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kwanza linalolenga wasiwasi wa kibinadamu. Hatua hii imeonyesha kuwa jamii ya kimataifa imetambua nafasi ya China katika suala hilo.

Kama alivyosema rais Xi, chanzo cha hali ya Israel na Palestina ni ukweli kwamba, haki ya utaifa ya Wapalestina, haki yao ya kuishi, na haki yao ya kurejea zimepuuzwa kwa muda mrefu. Hivyo, suluhisho la nchi mbili ndio njia pekee ya kusuluhisha mgogoro huo. China imekuwa ikiunga mkono wito wa Wapalestina wa haki zao kisheria na kupendekeza majadiliano ya kisiasa katika kutimiza amani endelevu na usalama katika kanda hiyo.


Mchango wa China katika maendeleo ya dunia

Mwaka 2023 utakuwa muhimu sana kwa nchi zinazojali ushirikiano wa kimataifa, na mwaka huu utaandikwa katika vitabu vya historia kwasababu nchi zote duniani zilizojiunga na Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” (BRI) lililotolewa na rais Xi Jinping wa China zinaadhimisha kumbukumbu ya miaka kumi tangu pendekezo hili lianzishwe.

Kati ya nchi zilizojiunga na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, nyingi zinazoteka bara la Afrika. Nchi 52 kati 53 za Afrika zilizoanzisha uhusiano wa kidiplomasia na China zimejiunga na BRI, pamoja na Umoja wa Afrika. Nchi hizo zimeshuhudia maendeleo makubwa katika sekta za ujenzi wa miundombinu, afya, nishati, kilimo na sayansi na teknolojia.


Mchango wa China katika kulinda utaratibu wa dunia

Mwezi Novemba, rais Xi Jinping wa China alifanya ziara rasmi nchini Marekani, ambako pia alihudhuria mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC) uliofanyika mjini San Fransisco.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, aliongea na wanahabari kuhusu mazungumzo kati ya rais Xi na rais Biden, na kusema ziara ya rais Xi nchini Marekani imevutia ufuatiliaji wa kimataifa, na hivyo kuongeza utulivu katika uhusiano kati ya China na Marekani, na kuleta chachu mpya katika ushirikiano wa Asia na Pasific, na kuleta nguvu chanya katika mazingira ya kikanda na kimataifa.