Zambia yaongeza hatua za kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu
2023-12-29 23:08:49| cri

Mamlaka za afya nchini Zambia zimetangaza kuwa hatua zimechukuliwa kuimarisha udhibiti wa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambao umeenea katika wilaya 12 nchini humo.

Waziri wa Afya wa nchi hiyo Sylvia Masebo amesema, kikosi kinachoundwa na sekta kadhaa kikiongozwa na Kitengo cha Usimamizi na Kukabiliana na Majanga kimeanzishwa ili kuhakikisha kuwa ugonjwa huo unadhibitiwa. Amesema hatua hiyo imewakutanisha pamoja wataalamu na kukusanya rasilimali muhimu kutoka wizara mbalimbali, na kwamba hatua hiyo pia imeongeza uwezo wa nchi hiyo kukabiliana kwa kina na mlipuko wa kipindupindu.

Amezitaja hatua zilizochukuliwa kuwa ni pamoja na kutoa maji safi na salama katika maeneo yaliyoathiriwa, hususan mji mkuu wa nchi hiyo, Lusaka, ambao umeathiriwa zaidi na mlipuko wa ugonjwa huo.