Wizara ya Ulinzi ya China yasema mazungumzo kati ya majeshi ya China na Marekani yamepata maendeleo ya kiujenzi
2023-12-29 10:12:36| CRI

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China Bw. Wu Qian amesema mazungumzo yaliyofanyika hivi karibuni kwa njia ya video kati ya maafisa waandamizi wa majeshi ya China na Marekani yamepata maendeleo ya kiujenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Bw. Wu alisema mjumbe wa Tume Kuu ya Jeshi la China Bw. Liu Zhenli alizungumza na Mwenyekiti wa Wakuu wa Majeshi la Marekani Bw. Charles Brown kupitia video tarehe 21 mwezi huu ambapo maafisa hao walibadilishana maoni kwa kina juu ya utekelezaji wa maafikiano yaliyofikiwa na marais wa nchi hizo mbili mjini San Francisco pamoja na masuala mengine yanayofuatiliwa kwa pamoja na pande hizo mbili.

Amesema China inatarajia kuwa Marekani itafanya juhudi pamoja na China kuhimiza uhusiano wa kijeshi kati yao kupata maendeleo thabiti katika msingi wa kuwa na usawa na kuheshimiana.