Mradi wa umeme JNHPP nchini Tanzania wafikia asilimia 94.78
2023-12-29 10:12:22| cri

Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Nishati wa nchi hiyo, Dkt. Doto Biteko amesema, utekelezaji wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), utakaozalisha megawati 2,115 kwa sasa umefikia asilimia 94.78, huku mashine mbili za kuzalisha umeme zimeshafungwa tayari kwa ajili ya kuanza kuzalisha umeme.

Dkt. Biteko amesema hayo alipofanya ziara ya kukagua mradi huo wilayani Rufiji. Amesema, itakapofika jumanne wiki ijayo, majaribio ya kwanza yatakuwa yamekamilika na itakapofika Februari 19 mwakani, majaribo ya pili yatakuwa yamekamilika tayari kwa kuanza kuzalisha umeme.