China yawaunga mkono wakimbizi nchini Sudan Kusini
2023-12-29 10:18:50| CRI

Waziri wa Mambo ya Kibinadamu na Usimamizi wa Maafa wa Sudan Kusini Bw. Albino Akol Atak Alhamisi amesema malori 6 ya China yaliyobeba vitu vya msaada kwa ajili ya wakimbizi na wanaorejea kutoka Sudan yanafika Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini.

Amebainisha kuwa hii ni hisani ya serikali ya China kwa watu wa Sudan Kusini, pia ni matokeo ya mawasiliano kati ya Sudan Kusini na jumuiya ya kimataifa na wahisani, ili kuisaidia serikali katika kukabiliana na wimbi la wakimbizi na wale wanaorejea kutokana na mapambano nchini Sudan.

Aliongeza kuwa serikali ya China itawapatia wakimbizi msaada mwingine wa dola milioni 1.4 za kimarekani, msaada huo utafika kabla ya mwishoni mwa Januari mwaka 2024.