Kenya yasema haitashindwa kulipa dola za Kimarekani bilioni 2 za Eurobond
2023-12-29 10:15:30| CRI

Kenya imesema italipa deni la dola za kimarekani bilioni 2 za dhamana ya Euro Eurobond katika wiki ya mwisho ya Juni 2024.

Waziri wa Hazina ya Kitaifa na Mipango ya Kiuchumi, Njuguna Ndung'u, alisema katika taarifa iliyotolewa Nairobi, kwamba nchi hiyo haitashindwa kulipa deni hilo kwani ina mpango kamili wa malipo ya huduma ya deni.

Amefafanua kuwa serikali ya Kenya hivi karibuni ililipa dola milioni 68.7 kwa riba ya dhamana ya Euro ambayo italazimika kulipwa mwezi Juni 2024, na kubainisha kuwa utatuzi wa malipo ya riba kwa wakati kwenye dhamana hizo sio tu umetoa ishara chanya kwa wawekezaji lakini pia umesababisha kupungua kwa mavuno kwenye dhamana hizo katika masoko ya fedha ya kimataifa.

Hata hivyo alisema kuwa nchi inatarajia mapato makubwa ya nje kutoka Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa, na taasisi nyingine za fedha za maendeleo kati ya Januari na Machi 2024.