Mkutano wa kazi za nje wa CPC wafanyika Beijing
2023-12-29 10:14:10| CRI

Mkutano wa Kazi za Nje wa Kamati Juu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC ulifanyika Beijing kuanzia Jumatano hadi Alhamisi. Rais wa China Xi Jinping, alitoa hotuba muhimu kwenye mkutano huo.

Katika hotuba yake, Xi alipitia kwa utaratibu mafanikio ya kihistoria na uzoefu wa thamani wa diplomasia ya nchi kubwa yenye umaalumu wa Kichina katika zama mpya, akafafanua mazingira ya kimataifa na wajibu wa kihistoria wa kazi ya nje ya China katika safari mpya, na kufanya mipango ya kina kwa ajili ya kazi za nje ya China kwa sasa na katika siku zijazo.