Rais Xi Jinping wa China amehutubia mkutano ulioandaliwa na baraza la mashauriano wa kisiasa la China kwa ajili ya kukaribisha mwaka mpya wa 2024.
Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi (CMC), alitoa hotuba muhimu kwenye mkutano wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) mjini Beijing.
Viongozi wengine wa chama na serikali ikiwa ni pamoja na Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng walihudhuria mkutano huo.
Viongozi hao wa chama na serikali iwaliungana na viongozi wakuu wa kamati kuu za vyama visivyo vya CPC na Shirikisho la Viwanda na Biashara la China, wawakilishi wa watu wasio na vyama, viongozi wakuu wa chama kikuu na idara za serikali, na wawakilishi kutoka makundi mbalimbali ya kikabila na sekta za jamii.
Kwenye hotuba yake Rais Xi amesisitiza kuendeleza nia kubwa ya kuijenga China kuwa nchi yenye nguvu na ufufuaji wa taifa la China katika pande zote, na kufanya China kuwa ya kisasa, kuwa ni kazi kuu ya Chama na nchi katika safari mpya katika zama mpya.
Rais Xi alitoa wito wa kuimarisha na kuendeleza umoja mpana wa kizalendo, na kusisitiza haja ya kuunganisha nguvu kupitia umoja, kuunda mafanikio makubwa kupitia kazi ngumu, na kujenga kwa pamoja sura nzuri juu ya mambo ya kisasa ya China.